February - Mwezi wa Kumiliki


MCH. CHRIS OYAKHILOME DSC DD

Hizi ni nyakati maalumu katika ufalme wa Mungu. 

Ni nini Mungu anatuambia kuhusu mwezi Februari?

Obadiah 1:17, Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.

Joshua 14:7-15 ....... 12 Basi sasa unipe mlima huu, ambao BWANA alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa yenye boma; yumkini yeye BWANA atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje, kama BWANA alivyonena. 13 Yoshua akambarikia, akampa Kalebu, huyo mwana wa Yefune, Hebroni kuwa urithi wake.....

Kalebu alimtaka Joshua atimize maneno ya Musa kama yalivyonena juu yake.  

Hebroni ilikuwa imejaa Majitu, lakini kwa sababu ya neno la Musa, Yoshua alimpa Kalebu Hebroni kama urithi wake.  

Kalebu alifukuza Majitu yote na kuchukua umiliki wa eneo lile. Alibadilisha urithi kuwa milki yake.  

Ni jambo moja kupewa au kukasimiwa urithi, na ni jambo lingine kuwa nao kama milki yako.

Juu ya mlima Sayuni kutakuwa na wokovu... Na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.

Huu ni mwezi wa Kumiliki.

Urithi ulikuwa ni wako tayari lakini sasa utaingia ndani yake kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. 

Kila Jitu litachinjwa.  

Kila upinzani utaharibiwa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Chukua umiliki katika Jina la Yesu!!!

Comments

Popular posts from this blog

Kongamano la Dunia Nzima la Mtandao wa Watafsiri wa Kimataifa

Maungamo ya Mwaka wa Ukombozi - 2024

Dhamini TeeVo Leo