Maungamo ya Mwaka wa Ukombozi - 2024


Fanya Ukiri/maungamo haya Kila siku ya Mwaka huu wa Ukombozi. 

Fanya madai ya kile alichokupa Bwana.

Nabadilisha vocha na kuponi zangu kuwa thamani halisi, zinakuwa mali halisi. 
Mimi ni neno la Mungu lililodhirika kuwa mwili kama Yesu alivyofanyika mwili.

Mimi ni udhihirisho wa Upendo wa Mungu na Neno lake

Tazama katika roho, na utaona kazi ya Mungu.
Waovu hawatashinda dhidi ya mwenye Haki.
Kwenda kanisani mwaka huu ni jambo la Utukufu. 

Ndani ya Kristo, hakuna kubabaika. Ndani yake maisha yangu ni imara.
Bwana ndiye Mchungaji wangu sitokuwa na uhitaji wowote. 

Sheria ya roho wa uzima inafanya kazi ndani yangu. Hakuna magonjwa, wala udhaifu, nguvu ya ukombozi inafanya kazi ndani yangu. 

Bwana amenishibisha kwa mambo mazuri, mimi ni wa thamani katika macho ya Bwana. 

Mwaka huu, nitakuwa na uzoefu wa udhihirisho wa Ufalme wa Mungu. Kuna udhirisho wa Kristo ndani yangu zaidi yangu.

Ninasukumwa na Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu ananiongoza kufanya vitu, kutenda mambo na shughuli mbalimbali zaidi ya fahamu zangu.

Tumeletwa katika udhihirisho wa Roho wa vitu ambavyo vilikuwa vimepita/ vimesahaulika kwa kitambo kirefu. 
Maisha yangu yatakuwa kama vile, mimi ni malaika..

Mimi ni Jibu. Mimi ni kifurushi cha majibu, kifurushi cha suluhisho, nabeba Majibu. Kuna udhihirisho wa hekima ya Kiungu mwaka huu ambao watu wengi wa Mungu hawajawahi kuung'amua wala kuiona kamwe. 
Hekima inaweza tu kuelezewa kwa Hekima.


Natembea kwenye afya ya kiungu, moyo wangu, mapafu yangu na kila ogani ndani yangu zinafanya kazi kwa ukamifu na ubora.
Wewe ni ni shangilizo na ushindi ndani yangu, eeh Bwana. 

#ukombozi #ushindi #badiliko #kurejezwa #kuwekwa-huru #kufunguliwa #kuachiwa #kuponywa #2024 #amedeuslive #pastorchris 

Comments

Popular posts from this blog

Kongamano la Dunia Nzima la Mtandao wa Watafsiri wa Kimataifa

Dhamini TeeVo Leo

Kubarikiwa Inamaanisha Nini!