Kongamano la Dunia Nzima la Mtandao wa Watafsiri wa Kimataifa
Kwa miaka kadhaa zaidi muongo Moja na nusu mtandao wa tafsiri wa Kimataifa umekua na kupanuka katika pembe zote nne za Dunia! Ndani ya kipindi hichi chote tumeweza kutafsiri nakala rhapsodi ya Uhakika katika lugha 7858 na kufikia nchi 242 za ulimwengu Mzima! Tumeweza kufikia miji na vijiji mbalimbali duniani kwa baraka ya nakala hizi za rhapsodi. Mabilioni ya watu wapata nakala hizi katika lugha wanazoweza kuzielewa kwa ufasaha zaidi na neno la Mungu liwewafikia wengi kuliko ilivyokuwa Awali! Tumekuwa na shuhuda kubwa na za kipekee kutoka kwa wafaidika wa Rhapsodi zinazogusa kila nyanja ya maisha, kuanzia Wokovu wa nafsi, afya, uchumi, amani na usalama katika familia, miji na Mataifa. Hakika rhapsodi ya Uhakika imekuwa ni malaika tarishi mwenye kubeba Habari njema za injili hai ya Bwana wetu Yesu Kristo. Katika mwaka huu 2023, mtandao wa tafsiri umeanda kongamano kubwa kabisa la Dunia Nzima, litakalo onyesha kazi mbalimbali za uinjilisti zinazoendelea kupit...