Kubarikiwa Inamaanisha Nini!

Watu wengi wanatumia neno nimebarikiwa au nataka niombe nibarikiwe, lakini bado wengi wao hawajui maana ya neno kubarikiwa. Kubarikiwa inamaanisha kusababisha kitu au mtu kufanya kazi kwa ubobevu wa hali ya juu zaidi kupita vipangamizi vyote. Kwa maneno mengine ule uwezo wa kile kitu au mtu aliokuwa nao ghafla unafunguliwa kutoka katika vizuizi na kila aina ya upinzani uliokuwepo kinyume nao na unaanza kutenda kazi kwa ubora wake wote. Tunaweza kuona hili katika injili ya Mathayo 14: 15-21 ambao Bwana Yesu alishukuru na kubariki mikate mitano na samaki 2 ambacho kilikuwa chakula cha kijana mdogo na kuwalisha umati wa wanaume 5000 bila kuhesabu wanawake na watoto. Mikate na samaki zilipokea nguvu ya kujizalisha bila kukoma, kiasi kwamba kila ikivunjwa na kugawiwa haikuisha wala kupungua. Huu ndio unapaswa kuwa uzoefu wa maisha yako kila siku, kwa sababu umebarikiwa kwa baraka zote za rohoni ndani ya Kristo Yesu. Wewe ni kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vy...